Sunday, November 12

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TRA


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) siku ya tarehe 03 Novemba, 2017 ilifanikiwa kumkamata Bwana Dunia Athumani Tema mkazi wa Buguruni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kujifanya Mtumishi wa TRA na kutoa huduma kwa mteja ndani ya Ofisi ya TRA Kariakoo – Gerezani Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo alifikishwa katika Kituo cha Polisi kilichopo Msimbazi, Dar es Salaam na kufunguliwa RB ya MS/RB/9263/17, KOSA: KUJIFANYA MTUMISHI WA UMMA (TRA).

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa wito kwa wananchi wote kutoa taarifa mara moja katika Vituo vya Polisi vilivyopo karibu, Ofisi za TRA zilizopo karibu au kupiga simu namba 0800780078 au 0800750075 endapo watakuwa na mashaka na mtu yeyote anaye wahudumia. Pia Mamlaka inawasisitiza wananchi wasikubali kupewa huduma zozote na mtu wanayemtilia mashaka.

TRA inapenda kuwakumbusha kwamba, watumishi wake wote wanapaswa kuvaa au kuwa na kitambulisho chenye majina na cheo wanapokuwa wanatimiza majukumu yao ya kila siku mahali popote.

‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’

Imetolewa na;
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Makao Makuu.
12/11/2017.

No comments:

Post a Comment