Saturday, November 4

Santi Cazorla: Mguu wa mchezaji wa Arsenal ulikuwa unaoza

Marca

Haki miliki ya pichaMARCA
Image captionMadaktari walitoa sehemu ya ngozi kutoka mkono wa kulia wa Cazorla na kuipandikiza kwenye kifundo cha mguu
Mchezaji wa Arsenal Santi Cazorla amesema madaktari walimwambia anafaa kushukuru sana iwapo ataweza kutembea tena baada ya kuambukizwa ugonjwa wa gangrini unaosababisha kuoza kwa sehemu ya mwili baada yake kufanyiwa upasuaji.
Mchezaji huyo wa miaka 32 kutoka Uhispania alicheza mara ya mwisho Oktoba 2016.
Alifanyiwa upasuaji kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia miezi miwili baadaye.
Lakini licha ya kufanyiwa upasuaji mara nane, kidonda chake hakikupona na badala yake alianza kuugua.
Cazorla ameambia gazeti la Marca kwamba ugonjwa huo ulikuwa "umekula" kano za kifundo cha mguu wake wa kulia.
"Sehemu ya ukubwa wa sentimita nane ilikuwa haipo," anasema.
Licha ya kutibiwa mara kadha kwa mafanikio, bado kulikuwa na wasiwasi kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Villarreal na Malaga angepoteza mguu wake kutokana na maambukizi kwenye damu yake.
Mara ya mwisho kwake kufanyiwa upasuaji sehemu hiyo ilikuwa 29 Mei.
Wakati huo madaktari walipandikiza ngozi kutoka kwa mkono wake wa kushoto - ambayo ina chale kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia.
Tangu wakati huo, Cazorla amekuwa akishiriki mazoezi na amesema anatarajia kuwa sawa kucheza mwakani.
Santi CazorlaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionChale kwenye mkono wa Santi Cazorla, sehemu ambayo kipande cha ngozi yake kilitolewa
Anasema amekuwa akipokea ujumbe kutoka kwa Andres Iniesta, David Silva na David Villa karibu kila siku.
Matatizo ya majeraha yalianza kumwandamana Cazorla alipovunjika mfupa mechi ya kirafiki dhidi ya Chile mnamo Chile Septemba 2013, na akaanza kuzoea kucheza akiwa na maumivu mguu wake wa kulia.
Desemba 2015, alifanyiwa upasuaji kwenye goti kabla ya kuumia kwneye kifundo cha mfuu mwaka mmoja baadaye.
MarcaHaki miliki ya pichaMARCA
Image captionPicha ya gazeti la Marca siku ya Ijumaa
Santi CazorlaHaki miliki ya pichaSANTI CAZORLA
Image captionSanti Cazorla aliandika kwenye Instagram baada ya upasuaji wa kwanza Desemba 2016

No comments:

Post a Comment