Madereva wanaokamatwa na polisi kwa kuendesha magari kwa kasi kubwa wanaweza kumnukuu Papa wanapoomba msamaha kwa polisi.
Katika mkutano na maafisa wa polisi wa usalama barabarani nchini Italia, Pope Francis aliwaomba waonyeshe "huruma " kwa madereva wanaovunja sheria za barabarani.
"huruma sio ishara ya udhaifu", alisema Papa. "Nawala haimaanishi kuacha kutumia nguvu ."
Aliongeza kusema kuwa polisi wanapaswa kutambua ni kwa nini mtu amefanya kosa.
Papa alikiri kuwa wakati mwingine husinzia akiwa kwenye maombi.
Hata hivyo alizungumzia kuhusu "ongezeko kubwa la makosa'' ya barabarani.
Alisema kuwa hali ya maisha ya watu kuwa na " haraka na ushindani " vimesababisha watu kuwaona madereva wenzao barabarani ''kama vizuwizi " ama washindani wao wanaopaswa kupitwa barabarani, na hivyo kuibadili mitaa kuonekana kama njia za mashindano ya magari ya Formula One".
Papa, ambaye amekuwa kiongozi wa kanisa Katoliki la Roma tangu mwaka 2013, pia aliwakosoa watu wanaotumia simu zao za mkononi wakati wanapoendesha magari.
"lazima tuangalie uwezo mdogo wa madereva wengi wa uwajibikaji, ambao mara kwa mara hawatambui madhara makubwa yanayotokana na kutokuwa kwao makini ," alisema.
Wiki iliyopita, Papa alibariki gari alilopewa kama zawadi ambalo sasa linapigwa mnada kwa ajili ya kupata pesa za msaada.
No comments:
Post a Comment