Katika mnada uliofanyika leo Alhamisi Novemba 9,2017 nyumba moja imenunuliwa kwa Sh900 milioni na nyingine kwa Sh1.1 bilioni.
Nyumba hizo ambazo zina kila kitu ndani, zipo umbali wa takriban mita 100 kutoka moja hadi nyingine. Mnada umefanyika kuanzia saa 5:58 asubuhi na ulidumu kwa wastani wa dakika tano kwa kila nyumba.
Mnada huo umeendeshwa na kampuni ya udalali ya Yono ukifanyika kwa mara ya pili baada ya wa kwanza wa Septemba 7,2017 kukwama kutokana na wateja waliojitokeza kutofikia bei iliyohitajika.
Akizungumza na Mwananchi jana Jumatano Novemba 8,2017 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yono, Scholastica Kevela alisema lengo la mnada ni kufidia Sh14 bilioni ambazo mfanyabiashara Lugumi anadaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Nyumba hizo mbili ni kati ya tatu ambazo zitapigwa mnada. Nyingine iko Upanga, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment