London, Uingereza. Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour Jeremy Corbyn amemtaka Malikia na wengineo kuomba radhi kwa kufanya uwekezaji ughaibuni kwa lengo la kukwepa kulipa kodi kwa sheria za Uingereza.
Corbyn aliuliwa katika mkutano wa CBI ikiwa Malikia anapaswa kuomba radhi kutokana na kufanya uwekezaji katika mataifa yanayoruhusu ukwepaji kodi.
Katika majibu yake Corbyn alisema mtu yeyote aliyeweka fedha zake mahali kwa lengo la kukwepa kodi sit u “aombe radhi kwa alichokifanya, bali atambue madhara yake kwa jamii".
Kufahamika kwamba Malikia amewekeza fedha kwa lengo la kukwepa kodi kumekuja baada ya shirikisho la kimataifa la vyombo vya habari vya uchunguzi kufichua nyaraka zilizopewa jina la Paradise Papers.
Nyaraka hizo zilizowekwa hadharani mwaka mmoja baada ya Panama Papers, zimemtaka Malikia kuwa miongoni mwa watu mashuhuri na matajiri waliokwepa kodi kwa kuwekeza visiwa vya Bermuda.
Baadaye msemaji wa Corbyn alifafanua matamshi ya bosi wake akisema kiongozi huyo hakumtaja Malikia moja kwa moja kumtaja aombe radhi bali anafikiri “mtu yeyote ambaye anaweka fedha kwenye maeneo yanayoruhusu ukwepaji kodi lazima atambue madhara yake kwa jamii ".
Makao makuu ya Malikia, Buckingham Palace hawakutoa kauli yoyote kuhusiana na taarifa ya nyaraka hizo kwamba asasi yake ya Duchy of Lancaster inayosimamia utajiri binafsi wa Malikia imekwepa kodi katika uwekezaji wake.
Msemaji wa Duchy of Lancaster alisema: "Tuna miradi mingi ya uwekezaji na michache kati ya hiyo inatumia fedha kutoka nje. Miradi yetu yote huwa inakaguliwa na ni halali. Malikia inalipa kodi kwa hiari katika kila mapato anayopata kutokana na uwekezaji."
No comments:
Post a Comment