Shalane Flanagan kwa mshangao amemshinda bingwa wa mara tatu wa mbio za marathon za New York, Mary Keitany kutoka Kenya siku ya Jumapili na kuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani kushinda mbio hizo.
Kwa upande wa wanaume wakenya waliwika pale Geoffrey Kamworor aliponyakua ushindi wake wa kwanza na kumshinda mwenzake Wilson Kipsang bingwa wa dunia wa mbio hizo kwa sekunde tatu.
Keitany alishashinda mara tatu mfululizo mbio hizo maarufu, lakini Flanangan mwenye umri wa miaka 36 alimpita Mkenya huyo kiasi cha maili tatu kabla ya kumalizika mbio na hakumona tena hadi mwisho akitumia saa 2 dakika 26 sekunde 53.
Mara ya mwisho kwa mwanamke Mmarekani kushinda mbio hizo za New York alikua Miki Gorman aliyenyakua taji mara mbili mfululizo 1976 - 1977.
No comments:
Post a Comment