Friday, November 24

MKURUGENZI WA IDARA YA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA AKUTANA NA MSAJILI WA UN-MICT


Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akizungumza na Msajili wa Mfumo wa Kimataifa wa kumalizia mashauri masalia ya iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (MICT), Dkt. Olufemi Elias alipotembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Novemba 2017. 
Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Caroline Chipeta na Maafisa mambo ya nje wakifuatilia mazungumzo. 
Maafisa walioambatana na Msajili wa UN-MICT wakifuatilia mazungumzo. 

No comments:

Post a Comment