Saturday, November 25

Misri yaapa kukabiliana na wauaji wa watu 235 Msikitini

Misri yaapa kukabiliana na wauaji wa watu 235 Msikitini
Image captionMisri yaapa kukabiliana na wauaji wa watu 235 Msikitini
Kikosi cha kijeshi cha Misri kimeanza mashambulio dhidi ya ngome za wanamgambo wanaodhaniwa ndio waliosababisha vifo vya watu wapatao 235 baada ya kuwashambulia katika eneo la rasi ya Sinai wakati walipokuwa wanatoka msikitini.
Waathiriwa wengi wa shambulio hilo lililofanywa na wanamgambo walikuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na maafisa wa jeshi waliokuwa wakitoka msikitini .
Serikali ya Misri imetangaza siku tatu za maombolezi kufuatia mauaji hayo.
Rais Abdel-Fattah al-Sisi ameahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wanamgambo hao.
Eneo hilo la Sinai hukumbwa na mashambulio ya mara kwa mara yanayofanywa na wanamgambo wanaopinga serikali ya Misri, na msikiti uliolengwa ni maarufu sana na waumini wa madhehebu ya kisufi na watu wa kabila la -Sawarka wanaosemekana kuunga mkono kikamilifu serikali ya rais rais Abdel-Fattah al-Sisi .

No comments:

Post a Comment