Sunday, November 12

MHANDISI MTIGUMWE ATEMBELEA KITUO CHA UKAGUZI WA MAZAO MPAKA WA HOLILI NA TARAKEA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe Leo Novemba 11, 2017 ametembelea Vituo vya ukaguzi wa mazao vilivyopo Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ili kujionea ufanisi wa utendaji kazi sambamba na kubaini Changamoto zinazowakabili ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa ushuru.

Katika ziara hiyo ya kikazi Mhandisi Mtigumwe ametembelea Kituo cha HOLILI na TARAKEA ambavyo vipo upande wa Tanzania ikiwa ni mpakani mwa Tanzania na Kenya.HOLILI ni moja ya mpaka kati ya Tanzania na Kenya ambalo upo umbali wa takribani Kilomita 25 Kutokea Himo Njiapanda huku Mpaka wa TARAKEA ukiwa umbali wa Takribani Kilomita 58 kutokea Himo Njiapanda.

Miongoni mwa Changamoto alizozibaini katika ziara hiyo kwenye Vituo vya ukaguzi wa Kilimo kwenye hivyo mipaka miwili ni pamoja na uduni wa vifaa vya kufanya kazi za Kiofisi, Kutokuwa na vifaa vya kufanya kazi ya kupimia Sampuli ya mazao katika Maabara ya Holili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mtigumwe amewataka watumishi wanaosimamia ukaguzi wa mazao kutojihusisha na vitendo vya upokeaji Rushwa kwani kwa mtumishi atakayebainika kufanya hivyo sheria zitachukuliwa haraka dhidi yake ikiwemo kufukuzwa kazi na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Mpaka huo wa TARAKEA una jumla ya Njia za panya 250 kutokea Mpaka wa Hororiri mpaka kufikia mpaka wa Namanga.Aidha, Alisema serikali inaendelea na juhudi mbalimbali za kuzikabili Njia za panya zote ili kubaini kila aina ya uhalifu unaofanywa ikiwemo magendo yanayopitishwa kinyemela.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisikiliza maelezo ya utendaji kazi katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua maabara ya upimaji wa mazao katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akifungua bomba ili kuona kama maji yanatoka wakati akikagua maabara ya upimaji wa mazao katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mpakani Mwa Tanzania na Kenya na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa Mazao cha TARAKEA.

No comments:

Post a Comment