Thursday, November 9

Mbunge wa Chadema aachiwa kwa dhamana


Mtwara. Mbunge Chadema  Cecil Mwambe  ameachililiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi jana.
Mwambe ametoka katika kituo cha polisi saa 6:45 akiongozana na mwanasheria wake na baadhi ya wafuasi wa Chadema huku kundi lingine la wana Chadema likiwa nje ya kituo cha polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari, wakili wa Mwambe Rainery Songea amesema mteja wake alikuwa anashikiliwa kwa tuhuma za uchochezi ambapo anadaiwa kutoa baadhi ya maneno ya uchochezi wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani juzi.
Songea amesema mteja wake amepewa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo tena Novemba 16 mwaka huu.
"Alishikiliwa kwa tuhuma za uchochezi ambazo wanasema alitoa maneno ya uchochezi katika mkutano uliofanyika  Novemba saba  katika kata ya railway. Uchunguzi unaendelea na jana waligoma kumpa dhamana lakini leo baada ya kujadiliana wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wamekubali kumpa dhamana na kumwambia arudi  Novemba  16 kwa hiyo tunamshukuru  ametoka, "amesema Songea
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chadema Mtwara mjini, Hassan Mpangile amesema kilichofanyika katika mkutano ni maneno ya kisiasa lakini wanaacha vyombo vya usalama viendelee na taratibu zake.
"Sisi kama wanasiasa hii kwetu makamanda inatupa mori zaidi ya kufanya kazi za kisiasa kwa matukio haya yanayoendelea,"amesema Mpangile
Leo Chadema kanda ya kusini wanategemea kuzindua kampeni za udiwani katika kata ya Mnacho wilayani Ruangwa mkoani Lindi ambako ni jimbo la waziri mkuu Kasimu Majaliwa.

No comments:

Post a Comment