Thursday, November 16

Mbunge asema majibu ya Serikali ni yale yale kila mwaka



Mbunge wa Songwe(CCM),  Philipo Mulugo
Mbunge wa Songwe(CCM),  Philipo Mulugo 
Dodoma. Mbunge wa Songwe(CCM),  Philipo Mulugo amekerwa na majibu ya Serikali na kusema yamekuwa ni yaleyale kila mwaka.
Mulugo alisimama na kuliambia Bunge kuwa hana mpango tena hata wa kuuliza swali la nyongeza kutokana na ukweli kuwa majibu ya Serikali kuhusu uvunaji wa mamba katika ziwa Rukwa yamekuwa hayaridhishi.
"Majibu ya Serikali ni yale yale kila mwaka na hata mwaka jana nilijibiwa hivyo kwa  hivyo bora kunyamaza tu," amesema Mulugo
Mwanzoni mwa mwaka jana mbunge huyo aliuliza swali kama hilo na katika swali la nyongeza aliangua kilio kwa kumbukizi kuwa mama yake mzazi aliuawa na mamba.
Akijibu swali la msingi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema uwindaji wa mamba hufanyika kwa kuzingatia takwimu kuhusu idadi ya mamba.
Hasunga amesema wizara imekuwa ikifanya utafiti wa wanyamapori na sensa hiyo inalenga kubaini idadi ambayo inawezesha upangaji wa kuvuna wanyama hao.

No comments:

Post a Comment