Jaji Sam Rumanyika alimhukumu adhabu hiyo msanii huyo baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Steven Kanumba bila kukusudia.
Kanumba ambaye pia alikuwa mwigizaji maarufu wa filamu ndani na nje ya nchi alifariki dunia April 7, 2012, kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo wake lijulikanalo kwa kitaalamu kama Brain Concussion, lililosababisha mfumo wa upumuaji kushindwa kufanya kazi.
Alipatwa na tatizo hilo wakati wa ugomvi ulioibuka baina yao usiku huo nyumbani kwake Sinza Vatcan, kutokana na wivu wa kimapenzi, baada ya kumtuhumu mpenzi wake huyo kuongea na simu na mwanaume mwingine.
Japo msanii huyo alikana shtaka la kumuua mpenzi wake huyo bila kukusudia akidai kuwa hahusiki kwa vyovyote na kifo hicho, bali mpenzi wake alijigonga ukutani ghafla wakati akimpiga kwa ubapa wa panga, lakini Jaji Rumanyika alimtia hatiani.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye Lulu kupitia kwa mawakili wake alianza mchakato wa kujinasua kutoka katika adhabu hiyo, baada ya kuwasilisha mahakamani hapo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani.
Mmoja wa mawakili wa msanii huyo, Peter Kibatala ameieleza Mwananchi leo Jumatatu kuwa hawakuridhika na hukumu hiyo na kwamba tayari waliwasilisha mahakamani hapo taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kumtia hatiani na kumhukumu adhabu hiyo.
“Tayari tumeshawasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa mahakamani (Mahakama Kuu) hivyo kilichobakia ni process (taratibu nyingine tu za kimahakama,” amesema Wakili Kibatala.
Kibatala amesema kuwa mbali na kukata rufaa pia watawasilisha maombi ya dhamana ili wakati anasubiria usikilizwaji na uamuzi wa rufaa yake akiwa nje.
No comments:
Post a Comment