Wednesday, November 22

Marekani yawakamata maafisa wa zamani wa juu wa Afrika kwa kadhia ya rushwa

Cheikh Gadio, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Senegal.
Chi Ping Patrick Ho raia wa China na Cheikh Gadio aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Senegal walipanga njama kutoa rushwa kwa maafisa wa juu wa Afrika ili kupata mikataba ya kibiashara kwa niaba ya shirika moja la nishati lenye makao yake Shanghai China na muungano wa mashirika makubwa ya fedha.
Walengwa wao walikuwa ni pamoja na Idriss Deby rais wa muda mrefu wa nchi yenye utajiri wa mafuta ya Chad, Sam Kutesa waziri wa mambo ya nje wa Uganda ambaye alikuwa rais wa baraza kuu la Umoja wa mataifa kuanzia 2014 hadi 2015.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ya wizara ya sheria ya Marekani iliyotolewa na waendesha mashitaka Jumatatu Ho na Gadio walijihusisha na mfumo wa miaka kadhaa wa kutoa rushwa Debby na Kutesa ili waweze kupata mikataba ya kibiashara kwa shirika hilo la nishati la mabilioni ya dola la wachina ambalo linafanya biashara ya mafuta na gesi pamoja na sekta ya fedha.
Mtandao wa rushwa uliundwa katika kuta za umoja wa mataifa mjini New York na kusambaa mabara kadhaa.
Shitaka hilo la kihalifu halijataja kampuni hiyo ya kichina inayohusishwa.
Naibu mkurugenzi wa kiongozi wa FBI William Sweeney amesema Ho na Gadio wanashutumiwa kwamba walikuwa wana nia ya kutoa fedha kwa viongozi wa nchi hizo mbili na kutofuata utaratibu wa kawaida wa kibiashara bila kujua kwamba kutumia mfumo wa benki wa Marekani kutawaponza.

No comments:

Post a Comment