Afisa mmoja mkuu nchini Iraq, amesema, makaburi kadhaa ya halaiki, yanayokisiwa kuwa na zaidi ya maiti 400, yamepatikana karibu na mji wa Hawija, mahali ambapo kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Islamic State, walifurushwa mwezi uliopita.
Gavana wa jimbo hilo la Kirkuk, amesema kuwa, makaburi hayo yaligunduliwa karibu na uwanja mmoja wa ndege, Kaskazini mwa Iraq.
Anasema kuwa baadhi ya maiti hizo zilikuwa zimevalishwa magwanda ya wafungwa, ambayo kundi la IS, huwavalisha wale ambao wamehukumiwa kifo, huku baadhi ya wengine walikuwa wamevalia mavazi ya kiraia.
Bw Said alisema kuwa ji ulikuwa umegeuzwa na kuwa eneo la kiwanyonga watu
Vikosi vya Iraq vimefundua makaburi maeneo ambayo wakati mmoja yalikuwa chini ya udhibiti wa Isamic Sate.
Mwaka uliopita shirika la AP lilichapisha takwimu za makaburi ya jumla ya sehemu 72.
Makaburi hayo yanaweza kuwa na miili ya kuanzia 5,200 hadi zaidi ya miili 15,000.
No comments:
Post a Comment