Chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki, operesheni hiyo iliyoanza Ijumaa Novemba 24,2017 imewezesha magari 21 kukamatwa.
Ibrahim Mwanga, meneja msaidizi mipango na matumizi ya rasilimali misitu kanda ya mashariki amesema leo Alhamisi Novemba 30,2017 kuwa upotevu huo unatokana na tathmini ya ukamataji wa wastani wa magari matatu kila siku yaliyotakiwa kulipia kodi ya Sh1.5 milioni kwa kila gari.
Mwanga amesema TFS inayashikilia magari 11 yaliyohifadhiwa katika ofisi za wizara jijini Dar es Salaam na mengine saba wilayani Kisarawe kwa ajili ya kupiga mnada magunia ya mkaa 790 yenye thamani ya Sh39.5 milioni baada ya siku 30 kuanzia leo.
Amesema mbali na idadi hiyo ya magari yanayoshikiliwa hadi sasa, yako mabasi yaliyokamatwa na kutozwa faini kabla ya kuachiwa.
Kwa mujibu wa Sheria ya Misitu namba 14 ya mwaka 2002 ni marufuku magari ya abiria kubeba mkaa ikielekeza faini inayoanzia Sh1 milioni hadi Sh5 milioni au kufunguliwa mashtaka mahakamani kwa wamiliki wa magari yanayokiuka vibali vya uendeshaji wa biashara hiyo
No comments:
Post a Comment