bunduki
Wednesday, November 22
Kwa Picha: Enzi ya Mugabe mamlakani
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Robert Gabriel Mugabealipata elimu yake katika shule ya misheni na baadaye akapata mafunzo kama mwalimu baada ya kuhitimu katika chuo kikuu cha Fort Hare ambako Nelson Mandela alisomea. Mwaka 1958, alikwenda kufanya kazi nchini Ghana
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Alikuwatana na Sally Hafron ambaye alimuoa mwaka 1961. Alikuwa mwanasiasa zaidi kuliko Mugabe kabla ya kufundishwa siasa na wanaharakati waliopiagania utaifa . Baadae alifungwa gerezani na serikali ya Rhodesian, na hakuruhusiwa kuhudhuria mazishi ya mtoto wake wa kiume
Haki miliki ya picha
GETTY IMAGES
Image caption
Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani mwaka 1974, alikuwa maarufu kama mmoja waviongozi wa vita vya msituni dhidi ya utawala wa wazungu wachache, pamoja na Joshua Nkomo (lkushoto)
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Walikubaliana kuweka silaha chini kwa amani katika mazungumzo yaliyoandaliwa na Uingereza. Waliunda vugu vugu la patriotic front - na jambo lililozishangaza waangalizi wa nchi za magharibi alishinda uchaguzi uliofanyika Februari 1980 kwa ushindi mdogo
Haki miliki ya picha
GETTY IMAGES
Image caption
Robert Mugabe alikuwa amewasili nchini Zimbabwe katika kipindi cha wiki sita tu kabla ya uchagaguzi baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka 10 . Akawa waziri mkuu prime minister, forming an inclusive government
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Katika miaka yake ya kwanza madarakani , alifurahiwa na viongozi kote duniani, miongoni mwao kiongozi wa Cuba Fidel Castro ambaye aliitembelea Zimbabwe mwaka 1986
Haki miliki ya picha
PA
Image caption
Pia alikuwa na uhusiano wa karibu na waziri mkuu wa Uingereza Margaret Thatcher - na awali allifuata sera ya maridhiano na maadui zake wakulima wa kizungu, na kuwaacha waendelee kukuza utajiri wao wa kiuchumi
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Alimuoa aliyekuwa mpiga chapa wake Grace Marufu, ambaye tayari alikuwa na watoto wake wawili, mwkaa 1996 miaka michache baada ya mke wake wa kwanza kufariki dunia . Miaka ya 1990 Zimbabwe iliingilia kati katika vita vya nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambavyo viliuathiri uchumi wa taifa
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Wakati serikali ya Tony Blair nchini Uingereza ilipojiondoa kwenye mazungumzo ya kudhamini mageuzi tata ya ardhi mwaka 1997 na baada ya Mugabe kupoteza kura ya maoni juu ya katiba mpya miaka mitatu baadae, wanamgambo wanaomuunga mkono Mugabe walianza kuvamia mashamba ya wazungu
Haki miliki ya picha
REUTERS
Image caption
Ni Wakati huu ambapo Mugabe alianza kuvalia nguo za rangi na kuachana Suti nyakati za kampeni
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Alikuwa ni mtu aliyependa sherehe kubwa ambazo zilikuwa zikiandaliwa mara kwa mara na chama tawala cha Zanu-PF kila mwaka kusherehekea siku yake ya kuzaliwa
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Katika sherehe hizo iliandaliwa keki ya pesa nyingi. Hii ilionyesha ni kwa namna gani waafrika wengi walimchukulia kama shujaa akihusudiwa kwa namna anavyo kabiliana na wakulima wa kizungu
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Hata hivyo umaarufu wake hususan katika maeneo ya mijni ulianza kushuka - na akapoteza ushindi katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa urais mwaka 2008, ambapo alishinda katika uchaguzi wa marudio baada ya chama cha Upinzani cha MDC kujiondoa kutokana na ghasia
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Vikwazo vilivyowekwa na Marekani pamoja na Muungano wa Ulaya vilimfanya Bwana Mugabe kugeukia sera za mashariki , ambapo alianzisha uhusiano wa karibu na Uchina katika uwekezaji. Amekuwa akienda Asia kwa matibabu yake - binti yake Bona (kati kati ) alisomea Hong Kong na Singapore
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Chama chake cha Zanu-PF kilishinda uchaguzi mkuu mwaka 2013, baada ya miaka minne ya serikali ya mgawanyo wa madaraka, iliyokuwa na sera ya utaifishaji ambayo ilikuwa na lengo la kuwapatia udhibiti wa uchumi wazimbabwe weusi . iliyosababisha kupotea kwa pesa taslimu na kusababisha maandamano mwaka 2016
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Hata hivyo vikosi vya usalama vilimuunga mkono Mugabe wakati wote- hadi pale mkewe Bi Grace alipoonyesha uroho wa madaraka jambo ambalo hawakuweza kulivumilia na kuvyo kuanzisha mchakato wa kuchukua madaraka ya nchi tarehe 15 Novemba 2017
Haki miliki ya picha
AFP
Image caption
Kulikuwa na shauku kuwa huenda ikawa ni mapinduzi, na Bwana Mugabe aliendelea na baadhi ya majukumu yake -licha ya kwamba umri wake ulionyesha kama mtu aliyesinzia wakati wa sherehe za mahafali ya chuo kikuu
Haki miliki ya picha
REUTERS
Image caption
Lakini baada ya maandamano makubwa wakati mchakato wa kupigwa kwa kura ya kutokuwa na imani nae ulipokuwa umeanza bungeni , Mugabe mwenye umri wa miaka 93- old akasalimu amri. Alijiuzulu baada ya kuwa madarakani kwa miaka 37 jambo lililoibua sherehe kubwa miongoni mwa raia wa Zimbabwe
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment