Sunday, November 26

KORTINI KWA KUKUTWA NA SEHEMU ZA SIRI ZA WANAWAKE

SERIKALI imemfikisha mahakamani mkazi wa Ipililo, Maswa, Salum Nkonja ama Emmanuel Nkonja (22), aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kukutwa na sehemu za siri za wanawake.
Nkonja alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na kusomewa mashtaka ya kumuua kwa kukusudia mtu asiyejulikana.
Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, alidai mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo kati ya Oktoba mosi na 30, mwaka huu.
“Mshtakiwa anadaiwa kumuua mtu asiyejulikana kwa kukusudia maeneo ya kati ya Kahama mkoani Shinyanga na Ubungo, Dar es Salaam,” alidai.
Hakimu Mkeha alimfahamisha mshtakiwa kwamba hatakiwi kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Katuga alidai upelelezi haujakamilika na kesi iliahirishwa hadi Desemba 8, mwaka huu.
Katika hatua nyingine, taarifa kutoka vyanzo vya uhakika zinasema mshtakiwa huyo alikutwa na viungo vya binadamu zikiwamo sehemu za siri za wanawake ambazo zimekaushwa.

No comments:

Post a Comment