Serikali yazindua Kamati Kuu ya maandalizi ya Africa Cup of Nation Under 17 (AFCON) yenye wajumbe ishirini na tano kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika nchini mwaka 2019.
Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe na kueleza kuwa uteuzi wa wajumbe hao wa kamati ulizingatia sekta muhimu zitakazo husika moja kwa moja katika kufanikisha mashindano hayo.
“Nawapongeza wajumbe wote kwa kukubali uteuzi huu maana kazi ya kamati hii si ya kulipwa bali ni kujitolea kwa manufaa ya nchi yetu na ninaimani kubwa kuwa tutafanya kazi nzuri na kwa kufanikisha mashindano haya tutakuwa tumelipa taifa heshima kubwa katika ulimwengu wa soka”,alisema Mhe.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika uzinduzi huo Mhe. Mwakyembe alisema kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo atakuwa yeye mwenyewe, Makamu Mwenyekiti atakuwa Mjumbe wa CAF na Rais wa heshima wa TFF Bw. Leodgar Tenga pamoja na Bw.Hendry Tandau kutoka Kamati ya Olimpiki nchini ambaye atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kamati.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Leodgar Tenga alitoa angalizo kwa TFF kuzingatia kigezo cha umri kwa watoto hao wanaowaanda kwa ajili ya mashindano hayo ili kuepuka kuvunja sheria kwani mashindao hayo yanalega vijana waliyochini ya umri wa miaka kumi na saba na si zaidi ya hapo.
Pamoja na hayo Kamati hiyo inawajumbe mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Paul Makonda,Mkurugenzi wa ATCL Bw.Ladislaus Matindi,Mohamed Dewji na wengine.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON under 17 mikakati mbalimbali itakayosaidia kufaikisha mashindano ya 2019 yatakayofanyika nchini (kulia) Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw Leodgar Tenga
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON Bw Leodgar Tenga (kulia) akizungumza katika kikao cha maandalizi ya mashindano yatakayofanyika 2019 nchini katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe na (kushoto ) ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw. Wallace Karia.
No comments:
Post a Comment