Friday, November 17

Jeshi la Zimbabwe laendelea kumshikilia Mugabe



Muuza magazeti akilipitia gazeti mjini Harare.
Watu wa Zimbabwe kwa siku ya pili leo wako katika hali ya wasi wasi wa kisiasa huku uvumi kuenea kuhusu ni lini au vipi rais Robert Mugabe ataachia madaraka.
Kwa mujibu wa Jeshi la Zimbabwe, Mugabe amezuiliwa nyumbani ili kuweza kuwasaka wahalifu ambao wamekuwa wakitumia mamlaka ya rais vibaya. Jeshi la nchi hiyo linasema Mugabe na familia yake wote wako salama.
Mugabe baada ya kutawala Zimbabwe kwa karibu miongo minne. Jeshi Jumanne lilichukua udhibiti wa taifa hilo bila umwagikaji wa damu.
Vyanzo vya habari vinasema kuwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amekataa kuachia madaraka ili kufungua njia ya Serikali ya mpito.
Ripoti kadhaa zinasema aliyekuwa makamu wake Emmerson Mnangagwa pamoja na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai wamerejea nchini baada ya kuwepo uhamishoni wakiwa tayari kushiriki kwenye serikali mpya.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Mugabe na mkewe Grace wameendelea kuzuiliwa nyumbani kwao mjini Harare.
Mchakato huo ulianza Jumatatu baada ya kiongozi wa majeshi generali Constantino Chiwenga kuonya kuwa angeingilia kati iwapo Mugabe hatosita kukandamiza wafuasi wa Mnangagwa ndani ya chama tawala ZANU-PF.
Dazeni ya watu wamekamatwa tangu Mugabe alipomfukuza kazi makamu wa rais Novemba 5. Mtawala huyo mkongwe alisema kuwa ana mpango wa kumweka mkewe katika nafasi ya makamu wa rais.

No comments:

Post a Comment