Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu
Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali
Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake
Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake
Uchumi ulidororeka baada ya mwaka 2000…
Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara ya uchumi
Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai
Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi
Ndoa yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza
Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake.
Jeshi limeonesha kumtaka Emmerson Mnangagwa aliyefutwa kazi kama makamu wa Rais na Mugabe mwezi Novemba
No comments:
Post a Comment