Uongozi wa hoteli hiyo pia umuagizwa kuwalipa fidia wateja, akiwemo Mwandishi wa habari wa Kituo cha Luninga cha ITV Mkoa wa Shinyanga, Frank Mshana aliyeibiwa kamera na kompyuta mpakato wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Elias Kwandikwa.
Nkurlu ametoa maagizo hayo leo Ijumaa baada ya kutembelea hoteli hiyo kutokana na uongozi kukaidi agizo la Mamlaka ya Mapato(TRA) la kulipa kiasi hicho kabla au ifikapo Julai 5.
“TRA walitoa siku 90 zilizomalizika Julai 5 kodi hii iwe imelipwa. Naona mlipuuza; sasa nawapa siku saba kuanzia leo mlipe, la sivyo nitaifunga huku hatua zingine za kisheria ikiwemo kuipiga mnada zikifuata,” ameagiza Nkurlu
Kabla ya kuuzwa na kubadilishwa jina kuwa Kahama Gold, hoteli hiyo ilikuwa ikiitwa Mongo Hotel.
Meneja wa TRA Mkoa wa Kodi wa Kahama, Jacob Mtemang’ombe amethibitisha hoteli hiyo kudaiwa Sh30 milioni inayotokana na kodi ya asilimia 10 ya mauzo yaliyofanyika zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
“Tayari tumekamilisha taratibu kadhaa za kiofisi ikiwemo kuwaandikia wahusika kuwakumbusha kulipa deni hilo; hatua zingine zitafuata kwa mujibu wa sheria,” amesema Mtemang’ombe
Akizungumzia suala hilo, meneja wa hoteli hiyo, Obedi Hussein amesema wanapitia nyaraka, kumbukumbu na sheria kubaini iwapo mmiliki mpya au wa zamani ndiye anastahili kulipa kodi ya mauzo.
“Ikibainika sisi wamiliki wapya ndiyo tunapaswa kulipa kodi hiyo, tutalipa mara moja,” ameahidi Hussein
Kuhusu wizi wa mali za wateja, meneja huyo amesema tayari uongozi umechukua hatua kadhaa kudhibiti hali hiyo anayodaiwa waliikuta waliponunua hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment