Sunday, November 26

Gavana asema uchumi wa Kenya uko imara

Rais Uhuru Kenyatta na Rais Raila Odinga
Uchumi wa Kenya umeonyesha ustahamilivu wa hali ya juu wakati nchi ikikabiliwa na hali tata ya kisiasa, Gavana wa Benki Kuu Kenya amesema Ijumaa.
Amesema nguvu ya uchumi huo inatokana na vyanzo mbalimbali vya uchumi huo na biashara ndogo na za kati nchini humo.
Pia amekadiria kuwa kukua kwa uchumi huo unaweza kufikia asilimia 5.1 mwaka huu—ambacho ni kiwango cha chini kilichofikiwa wakati wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.
Lakini amesema bado ukuaji huo ni juu ya asilimia 2.6 ya makadirio ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kenya ilikabiliwa na kipindi kirefu cha ukame kabla ya kutumbukia kwenye mzozo wa kisiasa wa muda mrefu, baada ya Mahakama ya Juu kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais, uliofanyika tarehe nane mwezi Agosti 2017.
Kenyatta, anatarajiwa kuapishwa Jumanne wiki ijayo, baada ya kutangazwa mashindi wa marudio ya uchaguzi, ambao ulisusiwa na mpinzani wake wa karibu, Raila Odinga.

No comments:

Post a Comment