Saturday, November 4

Dagaa wa Ziwa Nyasa waongezewa thamani


Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imeboresha thamani ya dagaa wanaovuliwa Ziwa Nyasa kwa kuwasindika na kuwaweka katika vifungashio maalumu.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Dk Oscar Mbyuzi alisema jana kuwa ili dagaa hao wapate soko la ndani na nje ya nchi uboreshwaji unahitajika.
Dk Mbyuzi alisema dagaa hao wanauzwa mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Morogoro, Mbeya, Tabora na Katavi.
Mvuvi Chalres Haule aliiomba Serikali kuwajengea kiwanda cha kukausha dagaa ili wakue kiuchumi na kufanya uvuvi kuwa endelevu.
Kaimu ofisa uvuvi wilaya ya Nyasa, Jacob Madondola alisema wameamua kuboresha soko la dagaa ili wauzwe kimataifa
Ofisa mfawidhi wa kituo cha udhibiti wa rasilimali za uvuvi, Godfrey Salaka alisema kwa kutumia boti za kisasa wavuvi wameweza kuvua samaki kwenye kina kirefu cha maji.

No comments:

Post a Comment