Buzwagi ambao umedumu takriban kwa miaka 10, ulikuwa tegemeo kubwa kwa mapato ya halmashauri ya mji wa Kahama.
Meneja wa mgodi huo, Stewart Hamilton aliliambia gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa ufungaji wa mgodi huo ni kawaida na hauna uhusiano na tatizo la uzuiaji usafirishaji makinikia nje ya nchi. Alisema wanafunga na kuondoka baada ya dhahabu kuisha, hivyo hawawezi kuendelea kuchimba kwa hasara.
Hata hivyo, Hamilton alisema maandalizi ya kufunga yameanza na ifikapo mwaka 2020 watakuwa hawapo, hivyo kutokana na wananchi wengi kwa miaka 10 kuishi kwa kutegemea uchumi kutoka ndani ya mgodi huo, watapitia kila mradi wakiwafundisha kuishi bila utegemezi wa mishahara.
Katika kuwajengea uwezo wananchi hao, alisema tayari wameweka maktaba katika mji wa Kagongwa kwenye halmashauri ya mji wa Kahama ambayo itakuwa na vitabu mbalimbali na machapisho yanayofundisha mbinu za ujasiriamali. “Katika maktaba hiyo ambayo tumeiweka kwa kushirikiana na Shirika la Read International, wananchi watapa fursa za kusoma bure vitabu hivyo,” alisema.
Wakati mgodi huo unafunguliwa ulikuwa na wafanyakazi 860, hali iliyosababisha kustawi kwa uchumi wa Kahama.
Naye mkurugenzi wa Read International, Magdalena George alisema kuna vitabu vinavyofundisha kilimo, ufugaji, ujasiriamali na shughuli mbalimbali za uchumi.
Akizungumzia hatua hiyo, kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama, Mary Chima alisema ofisi yake itahakikisha inasimamia vizuri maktaba hiyo ili ilete matokeo mazuri kwa jamii.
No comments:
Post a Comment