Tuesday, November 7

Bajeti yasaidia kuondoa uhaba wa dawa


Dar es Salaam. Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Tanzania haina upungufu wa dawa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuongezwa kwa bajeti.
Amesema hayo leo Novemba 7 mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Waziri Kivuli wa Afya Dk Godwin Mollel.
Waziri huyo kivuli alitaka kufahamu kwamba ni sababu gani dawa zinazotolewa kama msaada huwa zimekwisha muda wa matumizi.
“Nikuambie tu ukweli hivi sasa hatupokei misaada ya dawa ambazo zinakaribia kuisha muda wa matumizi na hatupokei aina ya dawa ambazo tunazo katika stoo,” amesema Ummy
Pia amesema bajeti ya dawa imeongezwa kutoka Sh.30 bilioni mwaka 2015 hadi Sh.261 bilioni mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment