Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amekamatwa na Jeshi la Polisi muda huu akiwa nyumbani kwake na amepelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa chama hicho, Abdallah Khamis imesema Zitto amekamatwa asubuhi hii Masaki wilayani Kinondoni, akidaiwa kutoa kauli za uchochezi wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi wilayani Temeke juzi.
No comments:
Post a Comment