"Safari za ndani na nje tutazipunguza tutaelekeza fedha kwenye mashine. Shirika hili linaweza kujiendesha vizuri. Pamoja na matatizo ya kifedha tuliyonayo kuna fedha sisi watumishi tunapata zitakwenda kwenye mashine,” amesema.
Waziri Kalemani amesema, “Tutakapopungukiwa tutaomba taasisi nyingine lakini awali ya yote nimeamua posho za wafanyakazi, semina na mimi mwenyewe zitakwenda kwenye mashine tusipate shaka kupata fedha ya kununua mashine."
Dk Kalemani amesema hayo leo Jumatatu alipotembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Mtwara.
Amewahakikishia wakazi wa mji wa Mtwara kuanzia sasa tatizo la umeme halitakuwepo.
Kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi na Mtwara, amesema jitihada zinaendelea ili kupata suluhisho la kudumu hadi ifikapo Novemba.
Waziri Kalemani amesema Serikali inayafanyia kazi matatizo ya kukosekana umeme wa uhakika katika mikoa hiyo.
Amesema leo Jumatatu zitapatikana megawati mbili na kufanya idadi ya umeme unaozalishwa kuwa megawati 12, hivyo kupunguza makali ya mgawo.
"Umeme unawaka hautazimika tena kwa Mtwara mjini kuanzia leo. Zipo mashine tisa na zinazofanya kazi sasa ni nne ambazo zinatoa megawati nane, juhudi zinaendelea kurekebisha mashine mbili na leo zitakamilika na tutakuwa na megawati nyingine nne hivyo kuwa na jumla ya megawati 12," amesema Dk Kalemani.
Amesema wananchi wilayani Masasi na Lindi wanapata mgawo wa saa nane na kuanzia sasa watapata wa saa kati ya nne na tano.
Waziri amesema wameagiza vipuli vya mashine zote tisa na wamekubaliana na mkandarasi zitafika ndani ya siku saba kuanzia leo Jumatatu.
Amesema wamekubaliana mashine zote zitaanza kufanya kazi na kuzalisha megawati 18. Mahitaji ya Lindi na Mtwara ni megawati 16.
"Nimekaa na makandarasi walikuwa wanatarajia mashine zinaweza kuja ndani ya miezi miwili, sasa tumekubaliana hizo mashine zifike ndani ya siku saba kuanzia leo kwa ajili ya vipuli vya mashine zote tisa,” amesema.
Dk Kalemani amesema, “Mashine zikishaingia wataalamu wetu walisema watazifunga kwa wiki tatu, nimekataa nimemwagiza mkurugenzi wa Tanesco wachukue wataalamu sehemu zozote za nchi waje hapa mashine zifungwe kwa muda wa siku tatu."
Pia, ameagiza mashine nyingine mbili za megawati nne ambazo zitaingia ndani ya siku 14 badala ya siku 90 kutokana na dharura iliyopo.
No comments:
Post a Comment