Tuesday, October 24

WALIMU WANAWAKE MANISPAA YA IRINGA WALALAMA KUTOPEWA NAFASI ZA KUONGOZA


Mgeni rasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza kuelekea mkutano mkuu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa.katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale akizungumza na walimu wanawake waliojitokeza kuelekea mkutano mkuu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa. Baadhi ya walimu wanawake waliohudhuria mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa.   Na Fredy Mgunda,Iringa. Walimu wanawake manispaa yaIringa walalamikia kutokuwepo kwa uwiano wa viongozi wanawake na wanaume katikasekta nyeti kama vile wakuu wa shule,maafisa elimu kata na wilaya wakati walimuwa wanawake ndio wengi hivyo inafifisha ndoto za kuwa viongozi kwa kuwawanauwezo wa kuongoza na kusimamia mambo mengi yakaenda kama yalivyopangwa. Hayo yamesemwa na walimuwanawake katika mkutano mkuu wa chama cha walimu wanawake kilichokuwakinaongozwa na katibu wa wilaya mwl. Fortunata Njalale katika ukumbi wa chuokikuu huria tawi la Iringa. Akisoma risala iliyoandaliwana kamati ya kitengo cha walimu wanawake MWL. Evon Mhewa alisema kuwa walimuwanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi katika kukamilisha majukumuyao. “Mwalimu wa kike anacheleweshewakulipwa madeni mbalimbali anayokuwa anaidai serikali maana bila kulipwa madeniyetu walimu hawawezi kufundisha kwa moyo kwa kuwa maisha yanakuwa magumu nakuwapelekea kubuni njia mbadala za kujiingizia kipato” alisema Mhewa Mhewa alizitaja changamotonyingine ni kutopata nyongeza ya mishahara ya kila mwaka na kusimama kwa mwakawa pili sasa,walimu kutopandishwa madaraja na wengine kupandishwa na kupokwamshahara pamoja na walimu wanawake kutokuwa na uwiano wa vyote katika sektanyeti. “Sisi walimu wa kike kwasasa tumesoma sana na tunaweza kuwa viongozi sehemu yoyote kwa kuwa tayaritumethibisha hilo kwa wanawake waliopewa kazi hiyo kwani wameifanya ipavyo nakuleta matokeo chanya kwa serikali hivyo tunaomba walimu wanawake tupewa nafasikatika ngazi ambazo tunastahili” alisema Mhewa. Akijibu risala hiyo mgenirasmi ambaye ni afisa elimu manispaa ya Iringa MWL .Tupe Kayinga alisema kuwani kweli walimu wanamadi mengi serikalini lakini akasema kuwa hiyo yoteimetokana na swala la uhakiki wa watumishi hivyo mchakato wa uhakikiukimalizika kila kitu kitakuwa sawa ninauhakika na hilo. “Unajua serikaliimechelewesha maswala mbalimbali ambayo ni kero kwa walimu kutokana na uhakikihivyo nawaomba walimu wawe na uvumilivu kwa kuwa kila kitu kitakuja kutengemaakama ilivyokuwa hapo awali” alisema Kayinga Kayinga aliwataka walimuwanawake kuendelea kusoma ili kuwa na elimu ndio itakayowapa nafasi mbalimbaliambazo zinashikiriwa na walimu wanaume hivyo bila kuwa na elimu walimu wanawakewataendelea kuongozwa na walimu wanaume kila sekta. “Najua kuwa walimu wanawakewanakipawa cha kuwa viongozi lakini mitaala mingi inataka walimu kuwa na elimuili kupata kuongoza sekta mbalimbali sasa inatubidi walimu kujiendelezakimasomo ili kukidhivigezo ambavyo mara nyingi imekuwa ni elimu ya walimuanayepaswa kupewa kitendo husika” alisema Kayinga Aidha Kainga aliwatakawalimu wanawake kugombea nafasi mbalimbali zinazojitokeza ili kupata nafasi zakuongoza na sio kila wakati kuwaacha walimu wanaume wakigombea pekee yao. “Tumieni fursa za kugombeanafasi zinazojitokeza msiogope wanawake mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kuogmbeakwa kuwa katika kada ya ualimu walimu wanawake tupo wengi hivyo kuanzia saiziwalimu wanawake amkeni mjitume kuhakikisha mnagombea” alisema Kayinga Naye katibu wa chama chawalimu wilaya ya Iringa mwl. Fortunata Njalale alisema kuwa mkutano huo ni wakikatiba kwa mjibu wa katiba ya chama cha walimu taifa hivyo katiba imewaagizakukaa na viongozi wa walimu wanawake kuzijadili changamoto za wanawake ilikuzipeleka katika mkutano mkuu wa wilaya. “Leo tupo walimu wanawakepekee yetu ili kubaini changamoto zetu na kuzipeleka kwenye mkutano mkuu nakuweza kuzitetea kwa pamoja ili kuboresha maslai ya walimu wanawake ambaowamekuwa wanakumbana na changamoto nyingi sana wawapo kazini” alisema  Njalale Njalale alisema kuwa walimuwanawake wamekuwa na mwamko wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuwawanauwezo wa kuwa viongozi na kuongoza kwa kupata matokeo chanya. “Tunakitengo cha walimuwanawake taifa kimetusaidia sana walimu wanawake kupata ujalisi na kuacha uogakugombea nafasi mbalimbali hivyo kwa sasa walimu wakiume wajipange sana maanawalimu wanawake tumedhamilia kugombea nafasi yeyeto itakayojitokeza katikachama chetu cha walimu” alisema Njalale 
Njalale aliwapongeza walimu
wanawake wanaothubutu kugombea nafasi mbalimbali kwa kuwa wamekuwa wakishinda
na wanafanya kazi ipasavyo na kusema kuwa walimu wanawake wanaweza bila
kuwezeshwa.

No comments:

Post a Comment