Tuesday, October 31

Urusi iliwafikia watumiaji milioni 126 wa Facebook Marekani

Facebook logo. File photoHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionNembo ya Facebook
Facebook imesema kuwa karibu watumiaji milioni 126 wa mtadao wa Facebook waliona yale yaliyokuwa yakichapishwa na Urusi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Mtandao huo wa kijamii unasema kuwa taarifa 80,000 zilichapishwa kabla na baada ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.
Nyingi ya taarifa hizo zilikuwa za kupotosha zilizohusu siasa.
Facebook ilitoa viwango hivyo kabla ya kikao cha Senate ambapo Twitter na Google wataelezea athari za Urusi katika mitandao hiyo maarufu.
Urusi mara kwa mara imekana madai kuwa ilijaribu kushawishi uchaguzi wa urais nchini Marekani ambapo Donald Trump alimshinda Hillary Clinton.
Viwango vya hivi punde vilivyotolewa na Facebook vimeonwa na shirika la Reuters na gazeti la Washington Post.
Taarifa 80,000 zilichapishwa kati ya Juni 2015 na Agosti 2017.
Faceboook inasema kuwa taarifa hizo zilichapishwa na kampuni ya Urusi yenye uhusiano na serikali ya Urusi.
A Facebook dislike button is seen in front of a a Twitter logoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTwitter na Facebook

No comments:

Post a Comment