Mmoja wa wagombea katika uchaguzi wa urais nchini Liberia na nyota wa soka George Weah amekiri kuwa na mawasiliano na kiongozi wa zamani wa taifa hilo Charles Taylor.
Bw Taylor anatumikia kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makossa uhalifu wa kivita baada ya kuhukumiwa na mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa.
Bw Weah amesema kuwa alipokea simu kutoka kwa mbabe huyo wa kivita, lakini akakanusha kwamba Charles Taylor ana ushawishi wa mambo nchini humo.
Wiki iliyopita, Bunge la Congress nchini Marekani liliidhinisha azimio la kushutumu juhudi zozote za mbabe huyo wa zamani wa kivita za kujaribu kuwa na ushawishi kwenye uchaguzi nchini Liberia kutoka gerezani.
George Weah ni mmoja wa wagombea 11 ambao wamejitokeza kutaka kumrithi Rais Ellen Johnson-Sirleaf ambaye anastaafu.
Makamu wa rais wa Johnson Sirleaf, Joseph Boakai, pia anawania katika uchaguzi huo utakaofanyika Jumanne tarehe 10 Oktoba.
Kuna mwanamke mmoja pekee aliyejitokeza kuwania, MacDella Cooper, ambaye alikuwa mwanamitindo lakini kwa sasa ni mfanyakazi wa hisani.
Jewel Howard-Taylor, 54, mke wa zamani wa Charles Taylor ni mgombea mwenza wa Bw Weah.
No comments:
Post a Comment