Twitter intarajiwa kuidhinisha sheria mpya za matangazo ya uchaguzi.
Mtandao huo wa kijamii unasema hatua hiyo inafuata shutumu za Urusi kuhusika katika uchakachuaji wa uchaguzi wa 2016 wa Marekani.
Akaunti 200 za watumiaji mtandao wa Twitter zilidhihirika kuwa na ushirikiano na ikulu ya Urusi Kremlin.
Marekani imetishia kuidhinisha sheria kutokana na ukosefu wa uwazi katika fedha zinazotumika katika matanagazo ya kisiasa katika mitandao ya kijamii.
Mtandao wa Twitter utakuwa na taarifa za nani aliyefadhili tangazo hilo la biashara, ni kiasi gani cha fedha kilichotumiwa, na ni nani aliyelengwa.
Wiki ijayoa kamati ya Intelijensia katika bunge la seneti litaanza kusikiza kesi kuhusu mitandao ya kijamii na propaganda.
No comments:
Post a Comment