Friday, October 20

Tillerson ajaribu tena kusuluhisha mgogoro wa Ghuba

Marekani itajaribu tena kuutatua mgogoro kati ya Qatar na Saudi arabia uliouchochea, wakati Waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson akielekea katika eneo hilo. Hata hivyo hana matumaini ya kuwepo mafanikio.

Waziri wa Mambo ya Nje Marekani, Rex Tillerson (Reuters/Y. Gripas)
Mjumbe huyo mkuu katika serikali ya Donald Trump anatarajiwa kuondoka Marekani mwishoni mwa juma hili kuelekea Saudi Arabia na pia Qatar kwa mazungumzo juu ya kile kinachotajwa kama kuvunjika kwa mahusiano ya nchi hizo mbili. Tillerson amesema baadhi ya pande husika zinaonekana kusita kuingia katika mazungumzo.
"Sina matarajio makubwa ya mafanikio kupatikana hivi karibuni," alikiri Tillerson  hapo jana alhamisi katika mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la Bloomberg. Rex Tillerson aliyewahi kuwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya nishati ya ExxonMobil, analielewa vyema eneo la Ghuba kutokana na uzoefu wake wa kujadili na viongozi wa kifalme wa nchi hiyo, juu ya mikataba au mipango ya mafuta na gesi.
Trump, aliyezidi kuchochoea mgogoro huo kwa kuungana na Saudi Arabia  na kuishutumu Qatar kwa kuunga mkono ugaidi, ametabiri kwamba mgogoro utasuluhishwa. Lakini mgogoro huu wa hivi karibuni wa kidiplomasia ni wa kukanganya, wakati washirika wa marekani wakitupiana lawama hata wakati Marekani ikijaribu  kushughulikia Iran na masuala ya ghasia zinazotokana na ugaidi.
Iran yafaidika na mzozo?
Mawaziri wa Mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Bahrain (Picture alliance/abaca/Stringer)
Mawaziri wa Mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Bahrain
Saudi Arabia, Bahrain, Umoja wa falme  za kiarabu na Misri zilivunja mahusiano ya kidiplomasia na Qatar mwzi Juni mwaka huu ikiishutumu kwa kuunga mkono ugaidi na kujipendekeza kwa Iran. Pande hizo  zimekuwa zikizozana kuanzia wakati huo licha ya juhudi kutoka Kuwait, na ziara ambayo haikuwa ya mafanikio ya Tillerson mwezi Julai mwaka huu, kujaribu kuwa mpatanishi katika mazungumzo ya kusuluhisha mgogoro.
Kundi hilo limekuwa  na nguvu katika uchumi wa Qatar iliyo tajiri kwa mafuta na kusababisha mvutano mpya katika eneo linaloyumba la Mashariki ya Kati, Uturuki ikijiunga na Qatar na Misri nayo ikionyesha uungaji mkono wake katika eneo la ghuba.
Wakati huo huo, Iran ambayo ni hasimu  wa Marekani huenda  ikafaidika kutoklana na  mfawanyiko huo katika kambi  hiyo ya mataifa yanayounga mkono nchi za magharibi na viongozi wa kijeshi  wa Marekani wana wasiwasi kuhusua athari zake za muda mrefu. Baada ya Trump kuunga mkono juhudi za kuitenga qatar licha ya kuwa mshirika wa kijeshi wa Marekani na  Marekani kuwa na  kituo cha kijeshi nchini humo,  badom kiongozi huyo wa Marekani hakutoa wito wa mazungumzo ya  kutafuta suluhisho.

No comments:

Post a Comment