Shirika la Afya Duniani (WHO), imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 10 kinara kwa watu wake kuugua ugonjwa wa kipindupindu.
Mataifa mengine yaliyotajwa ni pamoja na India ambayo ndiyo inayoongoza. Nyingine ni Haiti, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Bangladesh, Uganda, Msumbiji na Kenya, ambayo ilikumbwa na mlipuko mkubwa wa maradhi hayo kwa nyakati tofauti mwaka huu.
Katika ripoti yao iliyotolewa hivi majuzi, imesema kuwa sababu kuu ya kuandamwa na maradhi hayo ni kukithiri kwa mazingira machafu katika mataifa hayo.
Ripoti hiyo inasema kuwa watu bilioni 1.2 sawa na moja ya sita ya watu wote duniani wako hatarini kukumbana na maradhi hayo hatari.
Wakati Bara la Afrika likikumbwa na kadhia hiyo kutokana na unywaji wa maji yasiyofaa, hali ni tofauti kwa Ulaya na Amerika ya Kaskazini ambako mifumo imara ya maji taka imeyafanya mabara hayo yawe huru na kipindipindu kwa miongo mingi sasa.
Lakini watu zaidi ya bilioni mbili wamebakia bila maji safi na mifumo ya maji taka, hivyo, kipindupindu kinaendelea bila huruma kuathiri watu masikini zaidi duniani na ndani ya kila nchi athirika.
No comments:
Post a Comment