Kundi la Taliban nchini Afghanistan limekana lawama kutoka kwa mwanamume raia wa Canada kuwa mmoja wa watoto aliuawa na mke wake kubakwa wakati walikuwa wakishikwa mateka na wanamgambo hao.
Msemaji wa kundi la Taliban alisema kuwa kifo cha mtoto huyo kilitokana na matatizo ya uja uzito na familia hiyo ilikuwa katika eneop la kijijini na haikuruhusiwa kumuona daktari.
Pia alisema kuwa mtu huyo na mkewe, hakutenganishwa hata dakika moja ili kulinda usalama wao.
Alitaja lawama hizo za Joshua Boyle kama propaganda za serikali za nchi za magharibi.
Wanandoa hao walitekwa nyara wakati wakiwa safarini nchini Afghanistan mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment