Thursday, October 5

Sudan ''yakata uhusiano wake na Korea Kaskazini''

Rais wa Sudan Omar El Bashir anasakwa na mahakama ya ICCHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais wa Sudan Omar El Bashir anasakwa na mahakama ya ICC
Sudan imekata uhusiano wake na Korea Kaskazini ili kuafikia masharti ya Marekani ya kuondolewa kwa vikwazo, kulingana na gazeti la Uingereza la Financial Times.
Washington inatarajiwa kutangaza uamuzi wake wa iwapo itaiondolea Sudan vikwazo vyote mnamo tarehe 12 mwezi Oktoba.
Afisa mwandamizi wa serikali ya Sudan alisema wameafikia masharti yote na wanatarajia vikwazo hivyo kuondolewa.
Mnamo mwezi Julai rais Donald Trump wa Marekani alichelewesha uamuzi wake wa kuiondolea Sudan vikwazo vyote kwa muda wa miezi mitatu.
Vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Sudan viliwekwa baada ya taifa hilo kudaiwa ''kufadhili ugaidi''.

No comments:

Post a Comment