Polisi wa Israel walimkamata mwanamume mpalestina wiki iliyopiwa, baada ya kuchapisha salamu kwenye mtandao wa Facebook akisema "habari za asubuhi" kwa lugha ya kiarabu, lakini salamu hizo zikatafsiriwa visivyo kumaanisha "washambulie" kwa lugha ya kiyahudi.
Polisi walithibitisha kuwa mfanyakazi huyo alikamatwa kwa muda mfupi kwa kushukiwa kuchochea lakini akaachiliwa kabla ya makosa hayo kutambuliwa.
Chapisho hilo lilionyesha picha ya mfanyakazi huyo akisimama kando ya tinga tinga katika ukingo wa magharibi.
Magari kama hayo yametumiwa kuwashambulia waisraeli hapo awali.
Hakuna afisa anayezungumza lugha ya kiarabu aliombwa ushauri kabla ya mtu huyo kukamatwa
Chapisho hilo lililotiliwa shaka kwa sasa limefutwa.
No comments:
Post a Comment