Kwenye hotuba kali rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amekashifu vikali Muungano ya Ulaya kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.,
Ametishia kuwatimua wajumbe wa Muungano huo ndania ya saa 24, akisema kwa Ulaya ilikuw ikipanga njama ya raia Ufilipino, kutimuliwa kutoka Umoja wa Mataifa. Hata hivyo hakutoa ushahidi wowote.
Matamshi hayo yanakuja baada ya ujumbe wa nchi za magharibi kulaumu vita vya Durtee dhidi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Baadaye msemaji wa EU akasema kuwa ujumbe huo haikuwakilisha muungano huo.
Katika hotuba yake Duterte alisema: "Tutatolewa kutoka UN? Wewe mtoto wa malaya," Endelea.
"Mnaingilia kati masuala yetu kwa sabababu sisi ni maskini. Mnatoa pesa kisha mnaanza kuamrisha ni vitu gani vinastahili kufanywa."
Akihutubua ujumbe huo alisema, "Nyinyi ondoka nchi yangu ndani ya saa 24, nyinyi wote."
Hii si mara ya kwanza rais Duterte ameshambulia Muungano wa Ulaya, kufuatia shutuma dhidi ya hatua zake kali dhidi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Sera za Duterte za kuunga mkono mauaji ya kiholela katika vita dhidi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya zishutumiwa vikali kimataifa.
Polisi nchini Ufilipino wanasema kuwa wamewaua watu 3,850 katika oparesheni ya kupiga vita madawa ya kulevya tangu Bwa Duterte aingie madarakani mwaka uliopita.
No comments:
Post a Comment