Sunday, October 22

Rais Magufuli ateua Mbunge mwingine


Rais John Magufuli, amemteua Janeth Masaburi  kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Magufuli amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa ibara ya 66 (1)(e) ya katiba inayompa mamlaka ya kuteua wabunge 10.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ya Rais imeeleza kuwa Janeth Masaburi ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge.

No comments:

Post a Comment