Saturday, October 21

Posa ya Lulu yakataliwa na Baba yake

Baba Mzazi wa muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, Mzee Michael Kimemeta, amekataa kupokea posa ya binti yake huyo ambaye amekuwa akiwatoa udenda wanaume wengi kwa urembo wake.

Mzee Kimemeta amefunguka hayo alipokuwa akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba hatopokea posa ya mwanaume atakayekwenda kumuoa Lulu, kikubwa atakachoangalia ni furaha ya binti yake kwenye maisha yake.

“Suala la kuoana ni la watu wawili anayeoa na anaye olewa, yeyote atakayemleta sisi tunambariki, posa haiko kwenye msamiati wangu, siuzi mtoto, wala sitaki posa yoyote, posa yangu ni amani ndani ya nyumba yao, ndio posa watakayoniletea”, amsema Mzee Kimemeta.

Mzee Kimemeta ameonekana kuwa bega kwa bega na mwanaye kwenye kesi ya mauaji inayomkabili binti yake, iliyoanza kusikilizwa tena wiki hii.

No comments:

Post a Comment