Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imesema silaha hizo zimekamatwa na askari waliokuwa doria saa 4:30 usiku eneo la Msongola wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Oktoba 16, 2017 wakiwafuatilia watuhumiwa wa mauaji wilayani Kibiti waliokuwa wamepanda pikipiki moja wakiwa watatu.
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema hayo leo Jumatano Oktoba 18, 2017 alipozungumza na waandishi wa habari.
Amesema watuhumiwa hao watatu ambao hawajatambulika walipokuwa wakifuatiliwa na polisi waliongeza mwendo na kuingia barabara ya vumbi ambako walifyatua risasi.
Kamanda Mambosasa amesema askari waliwadhibiti watuhumiwa hao kwa kuwapiga risasi na kuanguka chini pamoja na pikipiki hiyo.
Amesema watuhumiwa hao wenye umri kati ya miaka 30 na 40 walipofikishwa katika Hospitali ya Temeke, daktari aliyekuwa zamu alithibitisha wamefariki dunia. Miili imehifadhiwa hospitalini hapo.
Katika tukio lingine, amesema watuhumiwa wawili wa ujambazi wameuawa eneo la Kibonde, Mbagala Zakheim ambako walipokea taarifa kutoka kwa wananchi kuwa walipanga kuvamia maduka ya Tigo-Pesa na M-Pesa.
Kamanda Mambosasa amesema watuhumiwa wakielekea eneo la tukio, wawili walipigwa risasi wakati wakiwashambulia askari na walipoteza maisha.
Amsema mtuhumiwa mmoja alitoroka na anaendelea kutafutwa na polisi.
Mambosasa amesema watuhumiwa walikutwa wakiwa na bastola ikiwa na magazine yenye risasi moja.
Pia, waliokota maganda matano ya risasi. Amesema bastola hiyo ilipakwa rangi nyeusi ili kuficha utambuzi.
No comments:
Post a Comment