
Rais wa Panama ametangaza siku ya Jumatano kuwa siku ya kitaifa baada ya nchi hiyo kufuzu kwa mechi za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanaa kabisa.
Juan Carlos Varela aliandika katika Twitter, "Sauti za watu zimesikika...Kesho ni siku ya kitaifa."
Panama ilishinda Costa Rica mabao 2-1 mjini Panama City siku ya Jumanne.
Rais alisema kuwa wafanyakazi wa umma na wale wa makampuni ya kibinafsi watapumzika na pia shule hazitafunguliwa.
Watu nchini Panama walisherekea usiku kucha baada ya ushindi huo.

Hata hivyo kumekuwa na utata ikiwa goli la kwanza la Panama lilivuka mstari wa goli.
Panama imejaribu kufuzu kwa kila kombe la dunia tangu mwaka 1978 lakini haijafanikiwa hadi sasa.
Nchi hiyo itashiriki katika mechi za mwaka 2018 ambazo zinaanza Urusi mwezi Juni mwaka ujao.
Marekani ilikuwa katika kundi moja la kufuzu kwa nchi za kaskazini na kati mwa Marekani, lakini ikashindwa baada ya kupoteza kwa Trinidad and Tobago.
Mexico na Costa Rica na walifuzu.
No comments:
Post a Comment