Tuesday, October 17

Ofisa magereza aliyekula uroda na mfungwa ajinyonga


Johannesburg, Afrika Kusini. Ofisa mmoja wa Chuo cha Mafunzo ya Wafungwa cha Losperfontein alijiua Jumatatu baada ya picha zilizomwonyesha akimpiga busu mfungwa kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, taarifa ya Idara ya Magereza imesema.
Idara ya huduma za magereza imeeleza kwamba ilifahamishwa kuhusu picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kwamba wakati wanafanya uchunguzi wa tukio hilo, wamekuja kugundua kwamba ofisa anayeonekana kwenye picha hizo tayari amejiua.
Kamishna wa magereza wa Limpopo‚ Mpumalanga na Kaskazni Magharibi, Mandla Mkabela‚ Mandla Mkabela amesema katika taarifa yao kwamba wameshtushwa na wamehuzunishwa mno na tukio hilo.
"Tunatoa salamu za rambirambi kwa familia na jamaa wa familia ya marehemu," alisema Mkabela.
Kamishna Mkabela ameelezea masikitiko yake kuhusu mkasa huo na akaongeza kwamba timu ya mameneja waandamizi na wanasheria imetumwa kwenye gereza hilo kutoa usaidizi wote muhimu unaohitajika kwa mfanyakazi huyo aliyefariki dunia.
“Tumetuma timu ya mameneja waandamizi na wataalamu wa mpango wa ushauri kwa wafanyakazi kwa ajili ya kutoa msaada wowote muhimu,” amesema Mkabela.
Mkabela, hata hivyo, amelaani tukio la usambazaji wa picha zinazodaiwa kuwa za ofisa huyo. "Hii inasumbua na ni jambo lililozuiwa kabisa,” alisema.

No comments:

Post a Comment