Nyalandu ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya awamu ya nne , ameeleza hayo katika akaunti zake mitandao ya kijamii ya Instagram, Twitter na Facebook huku akisema mswada huo atauwasilisha kwenye kikao kijacho cha Bunge.
Katika akaunti hizo Nyalandu ameandika: “Nakusudia kuwasilisha kwa Spika wa Bunge , Mheshimiwa Job Ndugai, azma yangu ya kuleta muswada binafsi wa sheria katika kikao kijacho cha Bunge itakayoweka sharti la kurejea upya mjadala wa Katiba Mpya ya Tanzania, kwa kuzingatia Rasimu ya Katiba ilivyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba,” .
No comments:
Post a Comment