Sunday, October 15

NASA yaomba vyombo vya kimataifa kuchunguza mauaji Kenya

Askari wa kuzuia fujo akitupa bomu la machozi wakati wa maandamano ya Nasa yanayoendelea dhidi ya IEBC nchini Kenya.
Wabunge wa Muungano wa upinzani, Nasa, wameanza kuviomba vyombo vya kimataifa kusaidia kuchunguza vitendo vya mauaji vinavyoendelea nchini Kenya.
Kwa mujibu wa upinzani mauaji hayo yanadaiwa kufanywa na polisi kwa wafuasi wa Nasa wakati maandamano dhidi ya IEBC yakiendelea kote nchini.
Seneta wa Siaya James Orengo, ambaye aliongoza wabunge 10 wa Nasa mjini Nairobi Jumamosi, ameviomba vyombo huru vinavyoisimamia polisi, Shirika la kimataifa la haki za bindamu Amnesty International, shirika la haki za binadamu Human Rights Watch, Tume ya haki za binadamu Kenya, kikundi huru kinachotoa huduma za kisheria za afya kuingia eneo la Bondo na kuchunguza mauaji ya Wakenya yanayofanywa na polisi.
“Tunaviomba vyombo vinavyosimamia haki za binadamu kwa uadilifu kuchunguza suala zima la kuwatafuta na kuwaua wafuasi wa Nasa kinyume cha sheria.
“Wanataka kuyageuza maeneo yaliyokuwa na wafuasi wa Nasa kuwa Biafra na Kosovo ya Kenya. Rais Uhuru Kenyatta na maafisa wa serikali yake lazima wajitayarishe kukabiliana na hatma ya jambo hili,” amesema Orengo.
“Iwapo unyama huu dhidi ya watu wetu utaendelea, sisi hatutakaa na kusubiri kuuwawa. Tutachukua hatua ambayo itaweza kuhakikisha tunajihami dhidi ya serikali dhalimu inayoangamiza watu wake,” amesema, akiongeza “tunamuonya Kenyatta kuwa afahamu kwamba anaipeleka Kenya mahali pabaya ambapo ni maangamivu kwa nchi hii kama tunavyofahamu.”
The MPs, who included Junet Mohamed (Suna East), Opiyo Wandayi (Ugunja), Tim Wanyonyi (Westlands) and Busia Woman Representative Florence Mutua, accused acting Interior Cabinet Secretary Fred Matiang’i and Police Inspector-General Joseph Boinnet of unveiling and executing a policy to eliminate Nasa supporters.
Wabunge hao ni pamoja na Junet Mohamed (Suna Mashariki), Opiyo Wandayi (Ugunja), Tim Wanyonyi (Westlands) na Mwakilishi wa Mwanamke wa Busia Florence Mutua wamemtuhumu kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i na Inspekta Jenerali wa Polisi Joseph Boinnet kwa kuanzisha na kutekeleza sera ya kuwamaliza wafuasi wa Nasa.
Siku ya Ijumaa, watu watatu wasio na silaha waliuawawa kwa kupigwa risasi wakiwa karibu na polisi huko mji wa Bondo wakati wafuasi wa Nasa wakiandamana kuipinga IEBC nchini Kenya.
Lakini Boinnet amedai kuwa watu hao watatu walipigwa risasi walipokuwa wakijaribu kuvamia kituo cha polisi, afisa mwengine alisema watu hao walikuwa wanaiba katika duka mojawapo.

No comments:

Post a Comment