Awali, jengo hilo lililojengwa na NSSF kwa Sh12.4 bilioni baada ya kuingia mkataba kati yake na jiji, lilikabidhiwa mwaka 2010 lakini deni hilo halijalipwa hadi kufikia Sh42 bilioni kutokana na mfuko huo kutengeneza faida ya Sh30 bilioni.
Hata hivyo, Mwita alisema juzi kuwa wameandaa kamati itakayoshughulikia suala hilo ili kuondoa mgogoro unaoendelea kati yao na NSSF.
Alisema makubaliano ya mradi wa ujenzi wa jengo hilo na NSSF ilikuwa deni hilo liishe kwa miaka kumi lakini limeonekana kupanda kutokana na kushindwa kulipa.
Meneja wa soko hilo, Ananias Kamundu alisema jengo hilo lina wafanyabiashara 1,430 na kwamba walianzisha minada sokoni hapo ili kuvutia wateja lakini haikufanikiwa kutokana na kuathiriwa na masoko ya jirani.
“Tuliweka mnada siku za Jumamosi na Jumapili, lakini kulikuwa kuna changamoto,” alisema
(Israel Mapunda)
No comments:
Post a Comment