Monday, October 30

Mmoja wa pacha waliotenganishwa India afungua macho

Conjoined twin boy after surgeryHaki miliki ya pichaAIIMS
Image captionMmoja wa pacha waliotenganishwa India afungua macho
Mmoja wa watoto pacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikana kwenye vichwa amefungua macho yake siku nne baada ya upasuaji wa kuwatenganisha nchini India.
Jaga, mwenye umri wa miaka miwili aliweza kuitikia ishara ndogo kama kusongesha mikono yake.
Ngugu yake, Kalia hata hivyo bado hajapata fahamu.
Watoto hao walizaliwa wakiwa wanatumia kwa pamoja mishiba na nyama za ubongo na upasuaji uliochukua saa 16 uliwatenganisha.
Watoto hao wote wako hali nzuri na madaktari wameridhishwa na vile wanavyoendelea hadi sasa, Professor Deepak Gupta, ambaye alishiriki katika upasuaji huo aliiambia BBC.
Conjoined twin after surgeryHaki miliki ya pichaAIIMS
Image captionMadaktari wanasema pacha hao wako hali nzuri
Conjoined twins at Delhi hospitalHaki miliki ya pichaAIIMS
Image captionPacha hao kabla ya upasuaji wa kuwatenganisha
Pacha hao wanaotokea kijiji kilicho mashariki mwa jimbo la Orissa nchin India, walishikana kwenye kichwa hali inayofahamika kama craniopagus.
Craniopagus hukumba mtoto mmoja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa na asilimia 50 ya wale wanaopatwa na hali hiyo hufariki saa 24 baada ya kuzaliwa.

No comments:

Post a Comment