Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo limesema miili ya watu 26 waliouawa katika shambulio lililofanywa na waasi mapema mwezi huu, imegunduliwa mashariki mwa nchi hiyo.
Marehemu wote hao ambao walikuwa ni raia isipokuwa mmoja, walishambuliwa katika eneo la Beni katika jimbo la Kivu kaskazini wakati wakisafiri na gari ndogo ya kukodi.
Mamlaka nchini humo zinasema kwamba zilishindwa kujua zilipo maiti hizo mapema kwa sababu ya mapigano makali yaliyokuwa yakitokea katika eneo hilo, ambako mamia ya watu waliuawa katika siku za hivi karibuni.
Jeshi la Congo na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakililaumu kundi la wapiganaji wa Uganda la Allied Democratic Forces ADF, kuhusika na mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment