Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi, (56) akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka aliyonayo.
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.
MHASIBU wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi, (56), leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka tisa matatu ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo wizi akiwa mtumishi wa umma, kujipatia fedha kwa njia ya uongo na utakatishaji wa fedha USD 150,000.
Mwendesha mashtaka wakili wa serikali, Wankyo Simon amedai Octoba 25 mwaka jana, katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania katika jiji la Maputa nchini msumbiji mshtakiwa Joyce kwa lengo la kufanya udanganyifu alighushi barua ya tarehe 25 October 2016 kwa madhumuni ya kuonesha kuwa ubalozi wa Tanzania nchni Msumbiji umeelekeza benki ya Millenium Bim, Maputo kuamisha USD 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Joyce Moshi.
Imedaiwa kuwa, akaunti zote hizo zipo katika benki ya Millennium Bim-Julius Nyerere Maputo, huku akijua kuwa siyo kweli.
Aidha mshtakiwa Joyce anayeishi Temeke anadaiwa Februari 10 mwaka huu huko huko Ubalozini nchini msumbiji, alighushi USD 100,000 na pia Aprili 12 mwaka huu alighushi tena USD 40,000.
Katika shtaka linguine Wankyo alidai kuwa, Oktoba 25, mwaka jana katika benki ya Millenium Bim-tawi la Julius Nyerere lililopo Maputo nchini Msumbiji.
Imedaiwa, mshtakiwa akifahamu na kwa njia ya udanganyifu aliwasilisha nyaraka ambayo ni barua ya tarehe Oktoba 25 mwaka jana kwa dhumuni la kuonyesha kuwa, ubalozi wa Tanzania nchni Msumbiji umeelekeza benki ya Millenium Bim, Maputo kuamisha USD 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na Joyce Moshi.
Pia aligushi barua ya Februari 10 mwaka huu ili kuhamisha USD 100,000 na barua ya Aprili 12 mwaka huuu ili kuhamisha USD 40,000.
Mshtakiwa Joyce anadaiwa pia kuwa, katika siku tofauti tofauti kati ya Oktoba 25 mwaka jana na Aprili mwaka huu, katika ofisi hizo za Ubalozi, akiwa muajiriwa wa utumishi wa umma wa kitengo cha fedha ubalozini hapo, aliiba USD 150,000 mali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Pia Joyce anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha pesa kwa njia ya udanganyifu kwa kujifanya kuwa ameelekezwa kutoa fedha hizo kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inaymilikiwa na Joyce Moshi huku akaunti zote hizo zimehifadhiwa kwenye benki hiyo ya Millenium.
katika shtaka la mwisho imedaiwa, katika tarehe tofauti kati ya Octoba 25 mwaka jana na Aprili 12 mwaka huu alijipatia USD 150,000 huku akijua kuwa fedha hizo ni matokeo ya kosa la kughushi.
Hata hivyo, mshtakiwa amekana shtaka hilo na amerudishwa rumande kwa kuwa kosa la utakaishaji halina dhamana na kesi hiyo imeairishwa hadi Octoba 30 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment