Monday, October 2

MBUNGE WA ILALA MUSSA ZUNGU AKAGUA UJENZI WA BARABARA ZA OLYMPIO NA MFAUME, UPANGA MASHARIKI, DAR ES SALAAM, LEO


Mbunge wa Ilala Mussa Zungu (kushoto)

NA BASHIR NKOROMO

MBUNGE wa Ilala, Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu, amesema ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa Barabara ya Olympio, katika kata Upanga Mashariki, huku akilalamikia ujenzi wa Barabara ya Mtaa wa Mfaume ambayo ujenzi wake umekwama. 

Zungu amesema hayo leo alipokagua maendeleo ya ujuenzi wa barabara hizo ambazo zinajengwa kwa kiwango cha lami chini ya usimamizi na gharama za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

"Kama mnavyoiona, barabara hii ya Olympio inayojengwa na kampuni ya kigeni ya China Railway Seventh Group (CRSG), imejengwa kwa kiwango kizuri kabisa, lakini hii ya Mtaa wa Mfaume yenye urefu wa mita 900, ambayo mkandarasi wake ni kampuni ya CASCO abayo ni ya mzawa mwenzetu 

imekwama kumalizika, Sasa tunamtafuta Mwenyekiti wa Halmashauri tujue nini hasa kimesababisha ujenzi wa barabara huu kukwama", amesema Zungu.

Amesema, wakati barabara ya Olympio yenye urefu wa mita 740  ujenzi wake umekamilika kwa kiwango kikubwa tangu Septemba 30, mwaka huu, ujenzi wa barabara ya  Mfaume umekwama hadi sasa kutokana na Mkandarasi kusimamishwa kuendelea kutokana na kuonekana anaijenga kwa viwango vya chini.

Wakala wa Ujenzi wa barabara ya Olympio kutoka kampuni ya CRSG Zhou Cunfei, alisema licha ya ujenzi kukamilika kwa asilimia 95, kampuni hiyo inamalizia sehemu chache zilizobaki na inainatarajia kuikabidhi rasmi Januari 2, mwakani.

 Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akizungumza alipokagua ujenzi wa Barabara ya Olympio, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam, leo. Watatu kulia ni Wakala wa Ujenzi wa barabara hiyo kutoka kampuni ya CRSG ya China, Zhou CunfeiWakala wa Ujenzi wa barabara ya Olympio kutoka kampuni ya CRSG ya China Zhou Cunfei akizungumzia wakati Zungu alipokagua ujenzi wa Barabara hiyo, leo. 
  Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akikagua ujenzi wa Barabara ya Olympio, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia ni Wakala wa Ujenzi wa barabara hiyo kutoka kampuni ya CRSG ya China, Zhou Cunfei
  Mwenyekiti wa CCM Kata ya Upanga Mashariki, akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo ya Olympio


 Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akihitimisha kwa kuzungumza na ujumbe wake baada ya kukagua ujenzi wa Barabara ya Olympio na ya Mtaa wa Mfaume, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

No comments:

Post a Comment