Mbowe amesema hayo leo Jumamosi kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.
Amesema kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa kambi rasmi ya upinzani ilikuwa inashauri wizara hiyo itenganishwe lakini ushauri wao haukufanyiwa kazi.
"Wizara ya Nishati na Madini ni wizara nyeti mno na mara nyingi tumekuwa tukiishauri Serikali iitenganishe wizara hiyo kwani ni kubwa na nyeti ila sasa wameona ushauri wetu unafaa na kuzitenganisha," amesema Mbowe.
Amesema suala siyo nani anafaa kuwa waziri na nani hafai kuwa waziri au ukubwa wa wizara ila suala ni kuona namna gani ya kuendesha Serikali ya Awamu ya Tano.
"Magufuli ajitafakari namna anavyoendesha Serikali kwani matakwa ya viongozi ndiyo yanakuwa maelekezo ya kuendesha nchi na hata mawaziri wanafanya kazi kwa matakwa ya mtu," amesema Mbowe.
No comments:
Post a Comment